MDOGO WA JOHN HECHE AUAWA NA POLISI.
Hali si shwari katika Mji wa Sirari wilayani Tarime jimbo la Tarime Vijijini ambapo mdogo wa Mbunge wa Tarime, John Heche, aitwaye CHACHA HECHE SUGUTA, ameuawa akiwa chini ya Ulinzi wa Polisi na ana jeraha la kuchomwa kisu. .
.
.
Ndugu wa marehemu wanasema wakati alipokamatwa na Polisi alikuwa mzima kabisa. Muda huu mabomu ya machozi na risasi vinafurumushwa kuwafukuza wananchi kutoka kituoni.
.
.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, RPC Mwibambe amekiri Askari wake kuhusika na mauaji hayo ya kijana huyo aliyezaliwa mwaka 1989. Chacha Suguta ni mdogo(upande wa Baba mdogo) wa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche(CHADEMA)
.
.
John Heche anasema kuwa kijana huyo alikamatwa na Askari wa Jeshi la Polisi usiku wa jana akiwa Baa akiwa mzima kabisa. .
.
Heche amesisitiza kuwa baada ya kufariki, Askari wa Polisi walitaka kuutupa mwili wake lakini ilishindikana kwa sababu eneo walilotegemea kuutupa kulikuwa na Mlinzi aliyewafukuza, ndipo walipoamua kuupeleka mwili wake kwenye chumba cha kuhifadhia maiti (Mortuary) ya Tarime.
.
.
#Mtatiro J
0 comments:
Post a Comment